Yanga sc yashinda dhidi ya Zalan fc, Yanga sc yatinga hatua ya kwanza ligi ya mabingwa Afrika, Yanga sc yatinga hatua ya kwanza CAF Champions league, Yanga imeefuzu hatua ya Kwanza ligi ya mabingwa Afrika leo, Yanga sc yasonga hatua ya kwanza ligi ya mabingwa Afrika.

Yanga sc yasonga hatua ya kwanza ligi ya mabingwa Afrika.

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuingia katika hatua ya kwanza katika ligi ya mabingwa Afrika (CAF Champion league) baada ya kushinda mechi zote mbili dhidi ya wapinzani wao Zalan fc kwa kuifunga timu hio, Klabu ya Yanga imeshinda kwa matokeo ya jumla ya mabao tisa,  Yanga sc 9-0 Zalan fc, Zalan fc ilifungwa mabao 4 katika mchezo wao wa nyumbani na kupoteza pia mabao matano katika mchezo wa ugenini.

Historia ya Yanga sc

Yanga sc ni timu ya mpira wa miguu iliyoanzishwa mwaka 1935, timu hii inashiriki ligi kuu Tanzania bara na ndio timu pekee ambayo imetwaa ubingwa Mara nyingi katika  ligi ya Tanzania ikiwa imebeba ubingwa Mara ishirini na nane(28).

Makao makuu ya yanga sc yanapatikana Dar es salaam Kariakoo Jangwani, timu hii inatumia uwanja wa Benjamin mkapa kama uwanja wa michezo yao ya nyumbani na imekuwa ikifanya vizuri katika uwanja huo.

Yanga sc imewahi kufiika katika hatua ya mkundi katika ligi ya mabingwa Afrika na kushindwa kuendelea katika hatua inayofuata ya robo fainali.

Yanga sc imetwaa ubingwa wa ligi ya Tanzania Mara ishirini na nane,  pia kombe la shirikisho ASFC Mara tatu, Ngao ya jamii Mara sita na idadi hii ya makombe ndio imefanya timu hii kuwa na idadi kubwa ya mashabiki.

Wapinzani wakubwa wa timu ya Yanga sc ni klabu ya Simba sc ambayo nayo inapatikana kariakoo msimbazi na zinapokutana timu hizi inakuwa ni moja ya mechi kubwa katika ukanda wa Afrika mashaiki .

Klabu hii ya yanga imeingia mkataba na kampuni ya michezo ya kubashiri Sportpesa kama mdhamini mkuu wa timu hio kwa mda wa miaka mitano, pia imaeingia mkataba na kampuni ya GSM mkataba huu unahusisha jezi na unakaa kwa mda wa miaka mitano .

Klabu hii ina uongozi ambao unaiongoza vyema klabu hii Raisi wa klabu ya Yanga sc ni  eng. Hersi said ambeye alichaguliwa kuwa raisi wa klabu hii.

Historia ya Zalan Fc Kutoka Sudan kusini

Zalan fc ni timu toka Sudan kusini, timu hii inashiriki ligi kuu ya sudani kusini na haina mafanikio makubwa katika ligi hii maana ndio imetwaa ubigwa kwa Mara ya kwanza katika ligi hio.

Zalan fc haina mafanikio makubwa kutokana na kukosa wadhamini katika timu yao na ligi yao ya Sudan kusini kwa ujumla, ligi hii ya sudani kusini haina wadhamini wowote kutokana na hali ya vita vinavyoendelea katika nchi hio na hata timu hizi zinazoshiriki ligi kuu ya Sudan kusini ni kutokana na mapenzi ya mpira walionayo wachezaji  hao.Yanga sc yasonga hatua ya kwanza ligi ya mabingwa Afrika

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here