Klabu ya yanga imeleta CEO mpya, klabu ya yanga sc imepata mtendaji mkuu, Yanga sc yapata mtendaji mkuu, Yanga sc imeshusha mtendaji mkuu, Yanga sc imeleta mtendaji mkuu mpya

Yanga sc imeleta mtendaji mkuu mpya

Raisi wa Klabu ya yanga sc Eng. Hersi said Leo katika mkutano wa waandishi wa Habari amemtambulisha  mtendaji mkuu baada ya kukaa kwa kipindi kirefu bila ya kuwa na mtendaji mkuu baada ya aliekuwa mtendaji mkuu senzo kumaliza mkataba wake na kuamua kuondoka, Leo klabu hii imemtambulisha mtendaji wake mkuu.

Rasmi Andre Mtine ndie mrithi wa senzo katika nafasi ya myendaji mkuu, mtendaji huyu ni raia wa Zambia na atakuwa akiitumikia klabu ya Yanga sc kwa kipindi cha miaka miwili kutokana na uzoefu alionao.

Mtendaji huyu ameanza kazi hii toka mwaka 1998, na amewahi kuhudumu katika klabu ya Zesco ya nchini kwao zambia, pia amewahi kufanya kazi na shirikisho la mpira wa miguu afrika CAF kama mjumbe wa kamati ya Fedha na ameitumikia klabu ya Tp Mazembe ya Congo kwa kipindi cha miaka kumi na mbili

Yanga sc ni klabu ya mpira wa miguu ya nchini Tanzania inayoshiriki ligi kuu Tanzania bars, makao makuu ya Yanga sc klabu ni kariakoo, Dar es salaam na inatumia uwanja wa Benjamin mkapa kama uwanja wa mechi za nyumbani, ni moja ya klabu bora katika ligi hio ikiwa imechukua ubingwa wa ligi ya Tanzania bara mara ishirini na nane na kushikiria rekodi ambayo hakuna timu nyingine iliowahi kuchukua ubingwa Mara nyingi kama klabu hii, pia klabu hii imewahi kufikia hatua ya makundi katika ligi ya mabingwa Afrika na kushindwa kuendelea mbele.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here