Uwanja we Sheikh Amri abeid wafungiwa, Uwanja we Sheikh Amri Abeid kutokutumika,Uwanja was Sheikh Amri Abeid hauruhusiwi kutumika,  Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wafungiwa kutumika

Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wafungiwa kutumika.

Bodi ya ligi kuu Tanzania bara (TPLB) imeufungia uwanja wa Sheikh Amri Abeid kutokana na kukosa vigezo na kanuni zilizotolewa na bodi hio ya ligi, uwanja huu unapatikana jijini Arusha na ni moja ya viwanja vikubwa katika ligi kuu ya Tanzania bara.

Sababu kuu ya kufungiwa kwa uwanja huu ni kukosa nyasi za kutosha katika eneo la kuchezea mpira yaani ( pitch ) kanuni hii ilitolewa katika kanuni za lessen za vilabu , kutokana na uwanjaa huu kukosa nyasi za kutosha inaweza kupelekea mazingira hatalishi kwa wachezaji wa mpira pamoja na kupunguza ubora wa picha za television na nyinginezo.

Bodi ya Ligi imezitaka klabu zilizokua zikitumia uwanja huo katika mechi za nyumbani kuchagua viwanja ambavyo itakuwa ikivitumia katika mechi zake za nyumbani timu hizo ni ” police Tanzania fc “(NBC premier league ) na ” Mbuni fc ” (championship).

Pia bodi ya ligi imeziisisitiza klabu zinazoshiriki championship kutunza miundo mbinu ya viwanja vyao vya nyumbani ili kuepuka usumbufu kama huu, kutokana na kuwa na viwanja bora itapeleka ligi yetu kukua na kufuatiliwa na watu wengi kutokana na kuwa na viwanja bora.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here