Mchezaji mpya asajiliwa na singida big stars
Singida big stars ni timu mpya katika ligi kuu Tanzania bara msimu we 2022/23, timu hii imeshiriki kwa mara ya kwanza ligi hio.
Timu hii inatumia uwanja wa liti ambao ulibadilishwa jina kutoka uwanja wa Namfua, uwanja huu unapatikana mkoani singida.
Singida big stars inamilikiwa na waziri wa fedha Mwigulu Lameck Nchemba.
Timu hii imefanya usajili mkubwa imetoa wachezaji nje ya nchi na baadhi ya wachezaji ndani na wengine ikiwatoa katika vilabu vikubwa Tanzania yaani simba na yanga.
Timu hii ilipopanda ligi kuu ilibadili jina awali ilikua ikiitwa DTB na kubadili jina na sasa inaitwa singida big stars.
Chimbuko la timu hii imetokea mkoani singida.
Usajili mpya wa singida big stars.
Mchezaji Escobar Miguel raia wa Argentina amesajiliwa rasmi na team ya singida bigs stars.
Mjezaji huyu anacheza nafasi ya mshambuliaji.