Singida Big Stars Kucheza na Pamba mechi ya Kirafiki

Timu ya Singida Big Stars ya Mkoani Singida inatarajia kucheza mchezo wa Kirafiki na Timu ya Pamba Sc ya Jijini Mwanza kwaajili ya kujiweka fiti wakati huu ambao timu ziko katika mapumziko kupisha mechi za kimashindano za timu ya Taifa.

 

Singida Big Stars ambayo imeanza vyema Ligi kwa kushinda mechi zake mbili za awali na kujikusanyia points sita katika nafasi ya tatu itacheza mchezo huo wa kirafiki katika kambi yao ya Mwanza ya siku 10.

 

Mechi hiyo itachezwa 27 August 2022 katika uwanja mkubwa zaidi kanda ya Ziwa uwanja wa CCM Kirumba kuanzia majira ya saa kumi kamili jioni.

 

TAARIFA KWA UMMA

Timu yetu itasafiri kesho Jumatano 24/08/2022 kuelekea Jijini Mwanza ambako tutaweka kambi kwa takribani siku 10 mfululizo. Sio Arusha tena kama tulivyopanga na kutangaza awali.

Tukiwa Mwanza, tunatarajia kucheza mechi ya kirafiki na Klabu ya Pamba FC @pambafootballclubofficial siku ya Jumamosi, itakayofuatiwa na mechi nyingine ya kirafiki tutakayoitangaza baadae.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by SINGIDA BIG STARS (@singidabsfc)

Ufahamu uwanja wa CCM Kirumba

Uwanja wa CCM Kirumba ni uwanja wa madhumuni mbalimbali mjini Mwanza, Tanzania. Una uwezo wa kuchukua mashabiki 35,000 na ni uwanja wa pili kwa ukubwa nchini baada ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

 

Mechi
Timu ya taifa ya soka ya Tanzania imecheza michezo mingi ya kirafiki katika uwanja huu.

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania ilicheza mchezo wa kirafiki katika uwanja huo dhidi ya Malawi tarehe 29 Machi 2015. Mchezo huo ulitoka sare ya 1-1.

Imekuwa ni nyumbani kwa timu za soka za Mwanza zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi Daraja la Kwanza Tanzania.

 

Fahamu kuhusu Pamba Sc

Pamba Sports Club ni klabu ya soka ya Tanzania yenye maskani yake jijini Mwanza iliyoanzishwa mwaka 1968 inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania.

Mwaka 1990 timu hiyo ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here