Simba yaingia robo fainali Asfc, Simba yatangulia hatua ya robo fainali kombe la Asfc, Simba sc imeingia hatua ya robo fainali Shirikisho, Simba yatinga Robo fainali kombe la shirikisho -Asfc

Simba yatinga Robo fainali kombe la shirikisho -Asfc.

Klabu ya soka ya simba sc imetinga hatua ya robo fainali katika kombe la shirikisho (ASFC) baada ya kushida mchezo wa hatua ya mtoano 16bora baada ya kuweza kuifunga klabu ya African sport mabao manne kwa sifuri, mchezo huu umechezwa katika uwanja wa uhuru.

Kombe hili la shirikisho ni moja ya kombe ambalo huibua vipaji vya vijana wengi ambao wanacheza katika ligi ya chini tofauti na ligi kuu na kuweza kufanya vijana hawa kupata klabu ambazo zinashiriki ligi kuu tanzania bara.

Mwisho wa michuano hii mshindi hupewa kombe na kupatiwa nafasi ya kushiriki kimataifa katika michuano ya CAF Confederation ambayo ni moja ya michuano bora barani Afrika na kupitia klabu zetu kushiriki michuano hiyo na kuweza kufanya vizuri timu zetu huweza kukua na kupanda katika viwango vya CAF.

Simba sc 

Simba Sports Club ni klabu ya soka ya Tanzania inayoshiriki ligi kuu ya tanzania bara na yenye makao makuu Kariakoo, Dar es Salaam, klabu hiyo iliyoanzishwa mwaka 1936 na kutengana na timu nyingine ya Tanzania Giants, ilipewa jina la Queens. Klabu hiyo imekuwa ikijulikana kama Queens, Eagles, na hatimaye Sunderland,  Waliitwa Simba mwaka 1971.

Simba SC ni moja ya klabu zenye ushindani mkubwa katika ligi hii ya tanzania na imewahi kushinda mataji 21 ya ligi na vikombe vitano vya ngao ya jamii ambayo huchezwa kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara  na imeshiriki mara nyingi katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Mbali na kuwa moja ya vilabu vikubwa Afrika Mashariki, wametwaa Ubingwa wa Klabu Bingwa ya CECAFA mara sita, pia klabu hii haina uwanja wa nyumbani hivyo inatumia  Uwanja wa Benjamin Mkapa kama uwanja wake wa mechi zake zote za nyumbani kimataifa na kitaifa pia imekuwa ikifanya vizuri ikiwa katika mechi zake za nyumbani na kuweza kupata matokeo mazuri katika uwanja huo na kujichukulia idadi ya mashabiki wengi wanaoishabikia timu hii.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here