Timu ya simba queen yatwaa ubingwa wa cecafa
Simba sport club ni timu ambayo makao makuu yake yapo kariakoo mtaa wa msimbazi, club hii ilianzishwa mwaka 1936.
Wapinzani wakuu wa timu ya simba sc ni yanga sc.
Timu ya simba sc inashirika ligi kuu Tanzania bara na imebeba makombe ya ligi hii.
Timu ya simba sc inatumia uwanja wa Benjamin William Mkapa national kama uwanja wake wa mechi za nyumbani.
Timuu hii ni moja ya timu yenye mashabiki wengi nchini Tanzania na timu hii imewahi kufika hatua ya robo fainali ligi ya mabingwa Africa (CAF CHAMPIONS LEAGUE).
Mzamini mkuu wa timu hii ni M-BET ambaye ameingia mkataba wa billion 26.1 kwa kipindi cha miaka mitano awali kabla haijaingia mkataba na M-BET mzamini mkuu alikua ni Tajiri MO DEWJ.
Pia simba sc ina timu ya wanawake inayoitwa Simba queen, timu hii ya simba queen inashiriki ligi kuu ya wanawake na imetwaa makombe mengi katika ligi hio na wapinzani wake wakuu katika ligi hii ni fountain Gate ndio wamekuwa wapinzani wakubwa wa timu ya simba queen.
Timu ya simba queen imetwaa ubingwa wa cecafa kwa Mara ya kwanza na inaenda kushiriki ligi kuu ya mabingwa Africa ligi ya wanawake.