Salum Abubakar na Farid Mussa kukosa mchezo dhidi ya Namungo, Sureboy na Farid kuikosa Namungo, Farid Mussa na Sure boy Kutokucheza mchezo wa namungo
Salum Abubakar na Farid Mussa kukosa mchezo dhidi ya Namungo.
Kiungo wa yanga sc Salum Abubakar sure boy na winga wa Yanga Farid Mussa watakosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo kutokana na majeraha waliyoyapata katika mchezo dhidi ya Tanzania prison na kuibuka kwa ushindi wa goli moja na kuchukua pointi zilizowafanya yanga kukaa kileleni.
Yanga sc itaingia dimbani kucheza na Namungo fc siku ya Tarehe 7 desember katika uwanja wa Majaliwa Stadium uliopo Mtwara.
Yanga, au Young Africans Sports Club, ni klabu ya soka ya Tanzania yenye makao yake makuu Jangwani, Dar es Salaam, Tanzania. Klabu hiyo ilianzishwa mwaka 1935 na inacheza michezo yake ya nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.