Sadio Kanoute kachukua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi kwa mashabiki, Sadio Kanoute mchezaji bora wa mwezi, Sadio Kanoute ameshinda kuwa mchezaji bora wa mwezi wa mashabiki, Sadio kanoute mchezaji bora wa mwezi November 2022 wa mashabiki
Sadio kanoute mchezaji bora wa mwezi November 2022 wa mashabiki.
Kiungo mkabaji wa klabu ya simba Sadio Kanoute amechaguliwa Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Mwezi November wa mashabiki wa klabu hio ya simba (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).
Kiungo Sadio Kanoute ameshinda tuzo hio baada ya kupigiwa kura na mashabiki wa simba na amewashinda viungo wenzake Mzamiru Yassin na Kibu denis ambao aliingia nao fainali kwenye kinyang’anyiro hicho.
Kwa ushindi huo Sadio Kanoute atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.
Sadio Kanoute(PUTIN)
Sadio Kanouté (aliyezaliwa 21 Oktoba 1996) ni mwanasoka Raia wa taifa la Mali ambaye anacheza kama kiungo wa klabu ya Simba sc iliopo nchini Tanzania.
Kanouté alicheza mechi yake ya kwanza ya kulipwa akiwa na timu ya taifa ya Mali katika mechi ya kufuzu kwa Ubingwa wa Mataifa ya Afrika 2020 na Mauritania mnamo 21 Septemba 2019.
Simba sc
Simba Sports Club ni timu ya soka ya Tanzania yenye makao yake makuu Kariakoo, Dar es Salaam.
Kwa kumuenzi Mtukufu Malkia wa Uingereza, klabu hiyo iliyoanzishwa mwaka 1936 na kutengana na timu nyingine ya Tanzania Giants, ilipewa jina la Queens. Klabu hiyo imekuwa ikijulikana kama Queens, Eagles, na hatimaye Sunderland, Waliitwa Simba mwaka 1971.
Simba SC imeshinda mataji 21 ya ligi na vikombe vitano vya nyumbani, na imeshiriki mara nyingi katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Mbali na kuwa moja ya vilabu vikubwa Afrika Mashariki, wametwaa Ubingwa wa Klabu Bingwa ya CECAFA mara sita. Uwanja wa Benjamin Mkapa ndio Simba inapocheza michezo yake ya nyumbani.
Simba ndio timu ya soka iliyo na akaunti ya Instagram iliyokua kwa kasi zaidi mwaka 2022, ikiwa na wafuasi milioni 1.9 na ongezeko la 89% kutoka mwaka uliopita.
Klabu hiyo ni miongoni mwa timu tajiri zaidi Afrika Mashariki, ikiwa na bajeti ya Sh Bilioni 6.1 (kama dola milioni 5.3) kwa msimu wa 2019/2020.