Mwanyi zahera katambulishwa na polisi tanzania, Mwinyi Zahera kocha mkuu wa polisi Tanzania, Mwinyi Zahera asainiwa na klabu ya polisi Tanzania, Polisi Tanzania yamtambulisha Mwinyi Zahera..

Polisi yamtambulisha kocha mwinyi Zahera.

Polisi Tanzania fc

Polisi Tanzania (Polisi Morogoro) ni klabu ya soka ya Tanzania iliyoko Moshi, Kilimanjaro. Msimu wa 2015/16 wanacheza Ligi Daraja la Kwanza Tanzania. Hapo awali walicheza katika kiwango cha juu cha soka ya kulipwa Tanzania, Ligi Kuu ya Tanzania.

Klabu hii imemtambulisha kocha mwinyi zahera kama kocha mkuu wa klabu hio.

Zahera anakuja polisi Tanzania  akitokea timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako alikuwa Msaidizi wa Florent Ibenge tangu Sep 30, mwaka jana.

Lakini Zahera pia amezifundisha DC Motema Pembe ya kwao, DRC tangu Machi 1, mwaka 2015 hadi Machi 10, 2016, akitoka kuwa kaimu kocha wa AFC Tubize ya Ubelgiji kati ya Oktoba 7 na Oktoba 23, mwaka 2014 ambayo alijiunga nayo akitoka kuwa Kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya DRC kati ya Agosti 14 na 28, mwaka 2017 chini ya Ibenge.

Alikuwa anafundisha AFC Tubize kwa mara ya pili, baada ya awali kuifundisha kama Kocha Mkuu kuanzia Julai 1 hadi Oktoba 20, mwaka 2010.

Zahera Mwinyi alizaliwa Oktoba 19, mwaka 1962 kabla ya kuanza soka mwaka 1975 akiichezea klabu ya Bankin ya Goma, Kaskazini mwa jimbo la Kivu, DRC hadi mwaka 1980.

Baadaye akaenda Kinshasa kucheza soka na kujiendeleza kielimu, akijiunga na Chuo cha Teknolojia (ISTA) huku akichezea klabu ya Sozacom hadi alipokutana na wakala wa wachezaji, Mbelgiji Karl Broken aliyemchukua na kumpeleka Ulaya kucheza soka ya kulipwa.

Mwinyi Zahera alicheza kwa misimu miwili Antwerp FC ya Ubelgiji kabla ya kumaliza mkataba wake na kwenda Ufaransa alikochezea timu za Daraja la Pili, Amiens, Beauvais na Abbeville hadi akastaafu soka.

Baada ya hapo akaanza kupata mafunzo ya ukocha, Zahera Mwinyi ambako alitunukiwa Diploma na leseni A ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) kabla ya kuifundisha klabu ya SC Feignies ya Ufaransa kuanzia mwaka mwaka 2000 hadi 2010 kwa mafanikio makubwa kabla ya kwenda Ubelgiji kuifundisha Tubize na baadaye jkutrejea nyumbani.

Thanks

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here