Picha ya Ommy Dimpoz na Cristiano Ronaldo,Picha ya Ommy Dimpoz na Bruno

 

Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutoka nchini Tanzania Ommy Dimpoz ameonekana kuotea picha na mastaa mbalimbali wa Manchester United akiwemo Star Cristiano Ronaldo na wengineo kibao mara baada ya mechi kati ya Manchester United dhidi ya Liverpool Old Trafford.

 

 


Msanii mwenzake wa Muziki ambaye pia ni shabiki mkubwa wa Manchester United Hamis Mwijuma Mwana Fa naye akatweet kwa Kusema

 

 

Picha za Ommy Dimpoz na Wachezaji wengine wa Manchester United

 

 

 

Singida Big Stars Kucheza na Pamba mechi ya Kirafiki

Wasifu wa Ommy Dimpoz

Omary Faraji Nyembo (amezaliwa 12 Septemba, 1987) ni mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania ambaye anajulikana kwa jina la kisanii kama Ommy Dimpoz. Ommy alianza kuvuma kwa wimbo wake wa Nai Nai aliomshirikisha Ali Kiba, Baadaye, Mama alioshirikishwa na Christian Bella, Me and You alioshirikishwa na Vanessa Mdee, Utamu alioshirikishwa na Dully Sykes, Hello Baby alioshirikishwa na Avril kutoka Kenya, Cheche, Achia Body, Tupogo, Ndagushima, Wanjera na Kajiandae. Ommy Dimpoz ni msanii mwenye masihara na maneno mengi ya kuchekesha. Sawa na Rayvanny wa WCB. Ommy ni moja kati ya wasanii ambao wanajali sana faragha za maisha yao.

Awali mwaka 2016 kulikuwa na gumzo kubwa baada ya Nay wa Mitego kumwimba vibaya Ommy kwenye wimbo wake na kumshutumu kama shoga.

Baadaye Ommy akajibu kwa kuonesha picha ya demu wake na ikaja kugundulika kuwa Nay wa Mitego ana kibamia.

 

Ommy ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Pozi kwa Pozi Entertainment ambayo meneja wake (Mubenga) aliachia ngazi mwaka wa 2016. Tangu wimbo wa Cheche (2017), amekuwa chini ya lebo ya Rockstar4000 ambayo iko chini ya Ali Kiba.

Mwaka wa 2018, ulikuwa mgumu sana kwa Ommy Dimpoz. Afya yake ilitetereka sana baada ya kufanyiwa vipimo Tanzania na kuonekana ana kansa.

 

Lakini baada ya kwenda Kenya kwa moja ya marafiki zake wanaofanya kazi pamoja katika muziki ili kufanyiwa uchunguzi zaidi, napo daktari wa huko alipendekeza apelekwe Afrika Kusini kwa uchunguzi zaidi. Akiwa Afrika Kusini aligundulika kama ana tatizo katika njia kuu ya kupitishia chakula.

 

Daktari wa Afrika Kusini walitengeneza njia mpya ya kupitishia chakula badala ya ile njia ya asili. Ili kufanikisha hili, ilibidi utumbo uvutwe juu.

 

Hivyo kina cha tumbo kimepungua kutoka hali ya umbo halisi. Hata uwezo wa kula umepungua, akila anashiba mapema sana tofauti na watu ambao hawajafanyiwa upasuaji huu. Kabla ya upasuaji, Ommy alilamikia sana kukosa pumzi, sauti kuwa chini na kadhalika. Hali halisi alifanyiwa upasuaji wa koromeo. Hali ambayo ilisababishwa na sumu iliyowekwa kwenye chakula. Ommy hajui ni wapi alifanyiwa hivyo

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here