Je Kisinda kutumika dhidi ya Al Hilal 8 October 2022?

Kumekuwa na maswali mengi miongoni mwa wanachama na wapenzi wa Yanga Sc kuhusiana na Tuisila Kisinda.

Klabu ya Yanga  inathibitisha kuwa Tuisila Kisinda atakuwepo miongoni mwa wachezaji  ambao Kocha Nabi anaweza kuwatumia katika mchezo huo.

Hapo awali dirisha la kwanza la CAF lilifungwa Agosti 15, 2022 kwa usajili wa mzunguko wa kwanza.

Hata hivyo CAF wakatoa tena fursa ya kuongeza wachezaji wengine mnamo Sept 15 kwa ajili ya Hatua ya pili.

Baada ya kukamilika kwa usajili wa Kisinda kuchukua nafasi ya Lazalous Kambole klabu iliongeza jina la Kisinda kwenye orodha hiyo ya wachezaji ambao watatumika kwenye hatua ya pili.

Hivyo ni rasmi kuwa Tuisila Kisinda atakuwa tayari kuwavaa Al Hilal ambao jioni ya Oktoba 6 wametua hapa nchini tayari kwa mchezo wa Jumamosi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here