Geita Gold imetolewa mashindano ya shirikisho Afrika, Geita Gold Yahindwa kuendelea Mashindano ya Shirikisho Afrika, Geita Gold Yapoteza Kwa Goli la Ugenini, Geita Gold yatolewa CAF cofendaratin September 17, Geita Gold Yatolewa CAF Cofedaration Cup.

Geita Gold Yatolewa CAF Cofedaration Cup

Timu ya Geita gold imeshinda mchezo wake wa nyumbani dhidi ya Hilal Al sahil ya sudani kwa mabao 2-1, na kushindwa kuendelea katika hatua ya kwanza kutokana na matokeo ya jumla kiwa Hilal Al sahil 3-3 Geita Gold, na kufanya klabu ya geita kutolewa kwa goli la ugenini walilofunga Hilal Al sahil dhidi ya Geita.

Katika mchezo wa awali klabu ya Geit Gold ilipoteza goli Moja kwa bila dhidi ya wapinzani wao.

Historia ya Geita Gold Football Club.

  • Geita gold ni timu inayotokea Tanzania katika mkoa wa Geita na makao makuu yake yapo Geita¬† timu hii inamilikiwa na mgodi wa madini uliopo Geita .

Kocha anyeifundisha timu hii ni Fred Felix minziro ambae ni raia wa Tanzania na aliwahi kucheza ligi ya Tanzania na kuchezea klabu kama yanga sc, ni moja ya makocha bora katika ligi yetu na ana lesseni A ya CAF .

Timu hii inatumia uwanja wa Nyakumbu kama uwanja wao wa nyumbani na wamekuwa wakiutumia uwanja huu vizuri na kushinda mechi nyingi za nyumbani.

Geita Gold Football Club imepanda ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2020/21, na baada ya kufanikiwa kupanda imefanya vizuri katika ligi kuu Tanzania bara na kumaliza katika nafasi ya nne katika ligi hio na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya CAF kwa Mara ya kwanza tangu timu hii ilipoanzishwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here