Fiston Mayele Aongeza Mkataba Yanga,Fiston Mayele yupo sana Yanga, Mayele aongeza Mktaba Yanga

Fiston Mayele Aongeza Mkataba Yanga

Klabu ya Yanga ambao ndiyo mabingwa wa ligi kuu soka ya Tanzania lakini pia ikiwa ndiyo wanaongoza kwa kulitwaa mara nyingi zaidi kombe la Ligi kuu kwa kutwaa jumla ya mara 28 wamemuongezea mkataba wake straika wao Fiston Mayele.

 

Mayele ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitajwa kutaka kutimkia nchini Afrika Kusini, wengine wakisema Morocco, Misri na nchini Sudan sasa atasalia Yanga mpaka msimu wa 2024.

 

Hii inakuja mara baada ya straika huyo raia wa Congo kukubali kuongeza mkataba wa Mwaka mmoja kusalia na wanajangwani hao, Awali Mayele Mkataba wake ulikuwa unaisha msimu wa 2022/2023.

 

Lakini kwa sasa ataendelea kuwepo Yanga Sc mpaka msimu wa 2023/2024, Kama ambavyo ilivyo kwa nyota wengine ambao waliongezewa Mkataba kama Mayele ambao ni Djuma Shaban aliyesajiliwa akitokea As Vita Club.

 

Mwingine ni Yannick Bangala Litombo ambaye naye pia atasalia mpaka msimu wa 2023/2024.

 

Yanga kupitia kwa Rais wake wa Sasa Engineer Hersi Said mmoja ya Marais vijana kabisa wamekuwa wakipambana kumalizana na wachezaji mapema kabla ya Mikataba yao haijaisha hali ambayo imekuwa inasaidia timu kuwa na malengo ya muda mrefu kutokana na wachezaji kuendelea kuwepo hivyo kurahisisha hata mipango ya Kocha.

 

Fiston Mayele anakumbukwa vyema sana na wapenzi ,wanachama na washabiki kwa Yanga kwa goli lake lililoipa Yanga ubingwa ngao ya Jamii msimu wa 2021/2022 na kisha tena magoli yake mawili yaliyoipa Yanga ubingwa wa ngao ya jamii 2022/2023 mechi zote wakicheza mbele ya watani wao wa jadi Simba Sc.

 

Mayele pia ndiye aliyekuwa mchezaji mwenye magoli mengi zaidi kwa Yanga sc katika msimu wa 2021/2022 katika ligi kuu soka ya Tanzania bara na mashindano yote lakini pia akishika nafasi ya pili nyuma ya George mpole .

 

George Mpole msomaji wa TanzaniaTrends.com alimaliza akiwa na Magoli 17 na kuwa kinara wa upachikaji mabao NBC Premier League huku Mayele akishika nafasi ya Pili kwa kuwa na Magoli 16 bao moja nyuma ya George Mpole

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here