Dokta Gembe wa Simba Afariki Dunia,Kifo cha Dokta Gembe,Daktari wa Simba Afariki Dunia,Kifo cha Daktari wa Simba Yassin Gembe
Aliyekuwa daktari wa timu ya Simba daktari Yassin Gembe amefariki Dunia leo mchana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Dokta Gembe mpaka umauti unamkuta alikuwa daktari wa timu ya vijana mara baada ya kuhamishiwa huko kikazi kutoka timu ya wakubwa ya wanaume.
TAARIFA YA SIMBA SC KUHUSU KIFO CHA DOKTA GEMBE
Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha aliyekuwa daktari wa timu yetu ya wanaume (Senior Team) ambaye kwasasa alikuwa daktari wa timu ya vijana (Youth Team), Dkt. Yassin Gembe ambacho kimetokea leo mchana kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
🕯 Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha aliyekuwa daktari wa timu yetu ya wanaume (Senior Team) ambaye kwasasa alikuwa daktari wa timu ya vijana (Youth Team), Dkt. Yassin Gembe ambacho kimetokea leo mchana kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. #NguvuMoja pic.twitter.com/ylsoW80TbW
— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) September 2, 2022
kuhusu Simba SC
Simba Sports Club ni klabu ya soka yenye maskani yake Kariakoo, Dar es Salaam Tanzania.
Klabu hiyo iliyoanzishwa mwaka 1936, iliyojitenga na Giant nyingine ya Tanzania, Dar Young Africans iliitwa Queens, kwa heshima ya Majesty, Malkia wa Uingereza. Klabu ilikuwa na mabadiliko kadhaa ya majina kutoka Queens hadi Eagles, kisha, Sunderland. Mwaka 1971 waliitwa Simba (Simba) kwa Kiswahili.
Simba SC imeshinda mataji 21 ya ligi na vikombe vitano vya nyumbani, na imeshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika mara nyingi. Pia ni moja ya vilabu vikubwa Afrika Mashariki, wakiwa wametwaa Ubingwa wa Klabu Bingwa ya CECAFA mara sita.
Simba wakicheza mechi zao za nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Mnamo 2022, Simba ilikuwa akaunti ya Instagram iliyokua kwa kasi zaidi kati ya vilabu vya soka, ikiwa na wafuasi milioni 1.9 na ukuaji wa 89% kutoka mwaka uliopita.
Klabu hiyo ni miongoni mwa timu tajiri zaidi Afrika Mashariki, ikiwa na jumla ya bajeti ya Sh Bilioni 6.1 (sawa na dola milioni 5.3) iliyozinduliwa kwa msimu wa 2019/2020.