Dodoma Jiji Fc yavunja mikataba ya benchi zima la ufundi, Dodoma jiji yaachana na benchi lake la Ufundi, Klabu ya Dodoma jiji Yavunja mikataba ya uongozi wa benchi la Ufundi, Klabu ya Dodoma jiji yaachana na makocha na benchi la Ufundi, Dodoma Jiji Fc Yavunja mkataba na benchi la ufundi

Dodoma Jiji Fc Yavunja mkataba na benchi la ufundi.

Klabu ya Dodoma Jiji fc imefikia makubaliano na ya kuvunja mkataba na kocha mkuu Masoud Djuma pamoja na benchi lake zima la ufundi, klabu hii toka imeanza msimu mpya wa Ligi kuu ya NBC imeshinda mchezo mmoja.

Klabu hii imewatakia kila la heri benchi lake la Ufundi na kuwashukuru kwa mchango mkubwa waliouonesha katika klabu hio.

Kwa sasa taarifa iliotolewa klabu hii itakuwa chini ya kocha wa vijana wa klabu ya Dodoma jiji Ndugu.Omary Mohammed Omary kwa mda mpaka itakapofanikisha kupata kocha mpya na benchi jipya la ufundi.

Dodoma Jiji Football Club ni klabu ya soka ya Tanzania yenye maskani yake katika Jiji la Dodoma, Imeanzishwa mwaka 2017 ikiwa inaitwa Dodoma fc na kubadilishwa Jina 2019 baada ya Dodoma kuwa Jiji na kuitwa Dodoma Jiji Fc na kuanza kumilikiwa na Halmashauri ya mji.

Klabu hii inatumia uwanja wa Jamuhuri katika michezo yake ya nyumbani uwanja huu unapatikana katika halmashauri ya jiji la Dodoma, imeanza kushiriki ligi kuu Tanzania bara katika msimu wa mwaka 2020/21.

 

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here