Diamond platnums September zanzibar

Kwa majina kamili msanii huyu Anajulikana kama Nasibu Abdul Juma. Ni msanii tuanaweza sema anaongoza afrika mashariki na mziki wake umepenya ulimwengu mzima. Ametokea nchi ya Tanzania na anafanya mziki aina ya bongo flava. Alijulikana kimataifa kupitia nyimbo yake ya “my number one”. Nyimbo hii ipo aina mbili kwani alifanya moja akiwa peke yake na nyengine akafanya na msanii Davido kutoka nchi ya Nigeria. Colabo hii ilileta manufaa kwa Diamond platnumz kwani alianza kupata kuchezwa kwa vyombo vya habari vya kimataifa.

Mnamo may 3 mwaka wa 2014, Diamond platnumz alivunja rekodi baada ya kushinda tuzo saba katiza tuzo za Tanzania music awards zikiwemo best male writer, best male artist, best song writer na pia best male entertainer of the year.

Diamond platnumz alianza kupenda mziki akiwa shule. Akiwa darasa la nne, Diamond alikuwa akiigiza wasanii wa Tanzania na wale wa kimataifa. Kuna wakati kwa tamasha alikuwa akitumbuiza watu kwa kuimba nyimbo za wasanii mbalimbali. Mamake Diamond almaarufu kama mama dangote alikuwa mstari wa mbele kusapoti kipaji Cha Diamond platnumz kwani hata alikuwa akimnunulia diamond albums za wasanii ili aweze kufuatilia nyimbo zao kwa kuyashika maneno yote ya hizo nyimbo. Akialikwa kwa sherehe, mama dangote alikuwa akimpeleka na zaidi alikuwa akimtafutia tamasha za kusaka vipaji akijua siku moja mwanawe atapata mtu wa kusapoti kipaji chake. Kwa sasa Diamond Platnumz Anajulikana ulimwengu mzima na ameachia zaidi ya nyimbo mia mbili. Utajiri wa Diamond Diamond Platnumz ndiye msanii anayesemekana kulipwa hela nyingi katika afrika mashariki. Pia ameorodheshwa bara nzima la afrika kama mmoja wa wasanii tajiri. Mziki wake umeuza sana katika mitandao ( music downloads. Amepiga music tour nyingi sana ulimwengu mzima na kampuni nyingi humtumia kwa matangazo ya biashara ikiwemo coca-cola ambayo ni kampuni kubwa duniani. Kumbuka Diamond Platnumz ndiye mwanzilishi wa WCB ( wasafi )Wasafi label inamuingizia mamilioni ya pesa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here