Chama kachukua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi kwa mashabiki, chama mchezaji bora wa mwezi, chama ameshinda kuwa mchezaji bora wa mwezi wa mashabiki.
Chama kawa mchezaji bora wa mwezi kwa mashabiki.
Kiungo mshambuliaji Clatous Chama, amechaguliwa Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Mwezi Agosti (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).http://Wasomiajira.com
Chama amewashinda viungo wenzake Pape Sakho na Sadio Kanoute ambao aliingia nao fainali kwenye kinyang’anyiro hicho.
Chama ameshinda kutokana na kupata kura nyingi kutoka kwa mashabiki zilizopigwa kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz kuanzia Agosti 29 hadi Septemba Mosi.
Kwa ushindi huo Chama atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.
Mchanganuo wa kura ulivyokuwa
Kura Asilimia Nafasi
Chama 1551 60.30 1
Sakho 506 19.63 3
Kanoute 516 20.06 2
Katika mwezi Agosti Chama amecheza mechi zote tatu sawa na dakika 231 akifunga bao moja na kusaidia kupatikana kwa mengine matatu.
Mchezaji huyu ni raia wa Zambia ambeye amekuwa mchezaji mzuri katika klabu yake ya simba na amekuwa akitoa mchango mkubwa kwa timu hio mpaka ilipofika hatua ya makundi ligi ya mabingwa Afrika.